Jeremiah 47

Ujumbe Kuhusu Wafilisti

1 aHili ndilo neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaishambulia Gaza:

2 bHili ndilo asemalo Bwana: “Tazama jinsi maji yanavyoinuka huko kaskazini,
yatakuwa mafuriko yenye nguvu sana.
Yataifurikia nchi na vitu vyote vilivyomo ndani yake,
miji na wale waishio ndani yake.
Watu watapiga kelele;
wote waishio katika nchi wataomboleza

3 ckwa sauti ya kwato za farasi waendao mbio,
kwa sauti ya magari ya adui
na mngurumo wa magurudumu yake.
Baba hawatageuka kuwasaidia watoto wao,
mikono yao italegea.

4 dKwa maana siku imewadia
kuwaangamiza Wafilisti wote
na kuwakatilia mbali walionusurika wote
ambao wangeweza kusaidia Tiro na Sidoni.
Bwana anakaribia kuwaangamiza Wafilisti,
mabaki toka pwani za Kaftori.
Kaftori ndio Krete.


5 fGaza atanyoa kichwa chake katika kuomboleza,
Ashkeloni atanyamazishwa.
Enyi mabaki kwenye tambarare,
mtajikatakata wenyewe mpaka lini?


6 g“Mnalia, ‘Aa, upanga wa Bwana,
utaendelea mpaka lini ndipo upumzike?
Rudi ndani ya ala yako;
acha na utulie.’

7 hLakini upanga utatuliaje
wakati Bwana ameuamuru,
wakati ameuagiza kuishambulia Ashkeloni
pamoja na pwani yake?”
Copyright information for SwhKC